Skip to main content

MISA TANZANIA WATEMBELEA MIRADI YA KIMKAKATI IKIWEMO DARAJA LA MAGUFULI

Wanachama wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Edwin Soko, wametembelea miradi ya kimkakati ya Serikali jijini Mwanza, ikiwemo ujenzi wa meli ya kisasa ya MV New Mwanza na Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo–Busisi), ili kujionea maendeleo yake na kuelewa mchango wake katika kukuza uchumi wa Taifa.

MISA TANZANIA WATEMBELEA MIRADI YA KIMKAKATI IKIWEMO DARAJA LA MAGUFULI
Studio Narration JAMBO FM

MISA TANZANIA WATEMBELEA MIRADI YA KIMKAKATI IKIWEMO DARAJA...

0:00 --:--

Wanachama wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tanzania), wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Edwin Soko, wametembelea miradi ya kimkakati ya Serikali jijini Mwanza, ikiwemo ujenzi wa meli ya kisasa ya MV New Mwanza na Daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo–Busisi), ili kujionea maendeleo yake na kuelewa mchango wake katika kukuza uchumi wa Taifa.

WAANDISHI WA HABARI WANACHAMA WA MISA TANZANIA WAKIWA KATIKA DARAJA LA JOHN POMBE MAGUFULI

Ziara hiyo imefanyika siku moja baada ya kongamano la wadau wa habari kutoka taasisi za umma na sekta binafsi lililofanyika jijini Mwanza, Oktoba 12, 2026, kujadili namna vyombo vya habari vinavyoweza kuchochea ukuaji wa uchumi, likiwa na kaulimbiu “Uhuru wa Vyombo vya Habari Kiuchumi.”

Kongamano hilo lilishirikisha wanachama 60 wa MISA Tanzania kutoka Kanda ya Ziwa, inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara na Kagera; Kanda ya Magharibi inayojumuisha Kigoma, Tabora na Katavi, pamoja na Kanda ya Kati inayojumuisha Singida na Dodoma, wakikutana na wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na sekta binafsi.

MWENYEKITI WA MISA-TANZANIA EDWIN SOKO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA ZIARA HIYO

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Soko ameipongeza Serikali kwa kuwekeza katika miradi hiyo mikubwa, akisema ina nafasi muhimu katika kuboresha usafiri na usafirishaji na kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi.

“Kwanza tumefurahishwa sana kuona mamlaka za nchi zinawekeza kwenye miradi mikubwa na ya kimkakati kama hii meli na daraja ndani ya Ziwa Victoria,” amesema Soko.

Ameiomba Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kutumia vyombo vya habari kutangaza miradi ya maendeleo ili wananchi wafahamu uwekezaji unaofanyika na manufaa yake kwa jamii.

“Ninaiomba Serikali ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan itumie waandishi wa habari kutangaza miradi ya maendeleo ili jamii ifahamu zaidi,” amesema Soko

AFISA UHUSIANO WA KAMPUNI YA MELI TANZANIA (TASHICO) ABDRULRAHIMAN ALLY AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUINGIA KATIKA MELI YA MV MWANZA

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO), Abdulrahman Ally, amesema meli ya MV New Mwanza inatarajiwa kuimarisha usafiri kati ya Mwanza na Bukoba mkoani Kagera, ikiwa na uwezo wa kubeba tani 400 za mizigo na abiria 1,200 kwa safari moja.

Amesema meli hiyo imezingatia pia mahitaji ya kijamii, ikiwemo uwepo wa lifti kwa ajili ya watu wenye ulemavu, pamoja na huduma zinazozingatia mahitaji ya wajawazito na wagonjwa.

AFISA UHUSIANO KAMPUNI YA MELI TANZANIA (TASHICO) ABDULRAHIMAN ALLY

Nalo Daraja la John Pombe Magufuli, linalounganisha Kigongo na Busisi, ni sehemu muhimu ya miundombinu ya usafiri katika Ukanda wa Ziwa Victoria, likilenga kurahisisha safari, kupunguza utegemezi wa vivuko na kuboresha usafirishaji wa bidhaa na huduma.

BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WAKITEMBELEA DARAJA LA MAGUFULI

Kupitia ziara hiyo, wanahabari wamepata fursa ya kujifunza kuhusu miradi hiyo na nafasi ya uandishi wa habari katika kuelimisha umma kuhusu uwekezaji, maendeleo ya miundombinu na fursa za kiuchumi zinazoweza kunufaisha wananchi.

WAANDISHI WA HABRI WAKISIKILIZA KWA MAKINI MAELEZO KUHUSU UTENDAJI KAZI WA MELI YA M MWANZA

BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WAKIFURAHIA UWEPO WAO KATIKA DARAJA LA JOHN POMBE MAGUFULI

WAANDISHI WA HABARI KATIKA DARAJA LA MAGUFULI

WAANDISHI WA HABARI WAKIWA NDANI YA MELI YA MV MWANZA

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.