Skip to main content

MIRADI ITAKAYOZINDULIWA 'KIZIMKAZI FESTIVAL' YAWAPA MATUMAINI WANANCHI

Wakazi wa Kizimkazi visiwani Zanzibar, wamesema Tamasha la Kizimkazi litakuwa zaidi ya burudani, kwa kuwa litaambatana na uzinduzi wa miradi ya maendeleo itakayowanufaisha kiuchumi.

Miradi hiyo itakayozinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi ni Jengo la Maendeleo la Shehiya Kibuteni, Barabara ya Kichakachindi–Mtondooni (KM 3.1), Hoteli ya Cave, Tenki la maji la lita milioni 1.5 na mradi wa nyumba za Bopar.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema tamasha hilo limekuwa likiongeza ajira za muda kwa vijana, kukuza biashara na kuboresha huduma za kijamii.

Wamesema, uzinduzi wa tenki la maji utasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji na kuboresha maisha ya wananchi.

Tamasha hilo lenye kaulimbiu ya 'Kizimkazi Kumenoga: Shangwe na Fursa' linatarajiwa kufanyika Agosti 12 hadi 14, mwaka huu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.