Jeshi la Polisi Nchini, limearifu kuwa linaendelea na uchunguzi wa kukusanya ushahidi kutokana na taarifa ya Hilda Newton aliyochapisha na kusambaza katika Mitandao ya Kijamii Aprili 10, 2026.
Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi iliyotolewa hii leo Aprili 22, 2026 imeeleza kuwa katika chapisho la Hilda pamoja na mambo mengine lilieleza kuwa, Serikali imepanga kumuua Tundu Lissu kwa risasi.

"Ili kukamilisha uchunguzi, Jeshi la Polisi linamwelekeza Hilda Newton afike katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai iliyopo katika Jengo la Makao Makuu Ndogo ya Polisi,"
"Iliyopo Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam tarehe 24.4.2026 saa nne (4) asubuhi ili aweze kuwasilisha ushahidi aliyosema na kutangazia umma kuwa anao," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Polisi wanaeleza kuwa, hatua hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 11 (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2023.

Discussion
Reader comments
0 contributions