Skip to main content

MIMBA ZA UTOTONI SI SALAMA, EPUKENI TAMAA - INSP. MWALONGO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, limetoa elimu kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari St. Bakanja Wilaya ya Manyovu Mkoani humo, kuhusu madhara ya mimba za utotoni.

Akitoa elimu hiyo hivi karibuni, Mkaguzi wa Polisi (INSP) Amani Mwalongo amewataka wanafunzi hao kuzingatia masomo na kuepuka mahusiano, kwani umri wao bado ni mdogo.

Amesema, mimba za utotoni nyingi husababisha kukatisha masomo changamoto za kiafya kwa mtoto wa kike na kuongeza mzigo wa maisha kwa familia hivyo kushindwa kufikia ndoto zao.

Aidha, INSP Mwalongo pia mewataka wanafunzi hao hususan wa kike kujitambua, kusikiliza ushauri wa wazazi na walimu, na kuepuka tamaa za vitu na mahusiano ya mapema.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.