Skip to main content

MILIONI 61 ZA MFUKO WA JIMBO KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO SHINYANGA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

MILIONI 61 ZA MFUKO WA JIMBO KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO SHINYANGA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ametoa fedha za mfuko wa Jimbo shilingi milioni 61, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake.

Fedha hizo zimegawanywa katika Kata zote 17 ambazo zipo Jimbo la Shinyanga Mjini, na kuelekezwa kwenye ununuzi wa vifaa vya ujenzi, ili utekelezwaji wa miradi hiyo ya maendeleo uanze mara moja, kwa ustawi wa wananchi.

Akizungumzia suala hilo  wakati wa ziara ya ukaguzi wa ufatiliaji fedha hizo  Katibu wa Mbunge huyo Samweli Jackson,amesema  kwasasa wanafuatilia iwapo  fedha hizo za mfuko wa Jimbo kama zimetumika ipasavyo kununua vifaa vya ujenzi, kwenye miradi ambayo imepagwa na viongozi wa Kata husika kutekelezwa, kwamba Katambi anataka kasi ya maendeleo kwa wananchi wake.

Jackson amesema, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Katambi ametoa fedha za Mfuko wa  Jimbo Sh.milioni 61, ili kuchochea kasi maendeleo katika Kata zote 17 Jimboni kwake, kwa kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Ziara ya leo tumefanya ufuatiliaji wa ununuzi wa vifaa vya ujenzi, kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia fedha za mfuko wa Jimbo Kata kwa Kata, na tumetembelea Kata zaidi ya 14, lengo ni kutaka miradi hii, jenzi zake zianze mara moja,” amesema Jackson.

Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo, amempongeza Mbunge Katambi, kwa kuendelea kuguswa na wananchi wa Shinyanga, na kuwapambania kuchochea kasi ya maendeleo, na sasa amegawa fedha za mfuko wa Jimbo katika Kata zote 17 kwa usawa.

Pia, ametoa maelekezo kwa watumishi wa Manispaa hiyo, kwamba vifaa vya ujenzi ambavyo vimenunuliwa kwenye miradi hiyo, vitumike ipasavyo na kuisimamia miradi yote itekelezwe kwa ubora na thamani ya fedha ionekane.

“kwenye hili nitakuwa mkali, nataka maeneo yote ambayo fedha zinatolewa kwa ajili ya utekelezwaji wa miradi ya maendeleo zisimamiwe kikamilifu, na kusiwepo na ubadhilifu wa aina yoyote, bali zitumike kwa uaminifu mkubwa na kutatua kero za wananchi,” amesema Kitumbo.

Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapindizi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga, amesema CCM wameridhika na utekelezwaji wa ilani ya CCM kupitia kwa Mbunge Katambi ,sababu wamekuwa wakijionea kwa vitendo utekelezwaji wa miradi ya maendeleo, na kuwaomba wananchi waendelee kukiunga mkono Chama hicho kwa maendeleo zaidi.

Nao Madiwani akiwamo Diwani wa Kizumbi Rubeni Kitinya wamemshukuru Katambi, kwa kuendelea kutoa fedha kwenye Kata zao, na kuchochea kasi ya maendeleo kwa kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Baadhi ya wananchi wa Shinyanga akiwamo Aghatony Matondo kutoka Ngokolo, wamesema wamefurahi kuona ujenzi wa Zahanati kwenye Kata hiyo unaanza, kilio ambacho kilikuwa cha muda mrefu, na sasa kina kwenda kutatuliwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.