Skip to main content

MILA POTOFU: WATATU WALIOMTOROSHA MWANAFUNZI WADAKWA MORO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu watatu wanaotuhumiwa kumtorosha Mwanafunzi wa kidato cha nne (jina limehifadhiwa) wa Shule ya Sekondari Sokoine Memorial na Mkazi wa Sokoine Shule.

MILA POTOFU: WATATU WALIOMTOROSHA MWANAFUNZI WADAKWA MORO
Studio Narration JAMBO FM

MILA POTOFU: WATATU WALIOMTOROSHA MWANAFUNZI WADAKWA MORO

0:00 --:--

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu watatu wanaotuhumiwa kumtorosha Mwanafunzi wa kidato cha nne (jina limehifadhiwa) wa Shule ya Sekondari Sokoine Memorial na Mkazi wa Sokoine Shule.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro iliyotolewa hii leo Oktoba 30, 2026 imewataja watuhumiwa hao kuwa ni kandolo Rosingo Kibasisi (56) Sokoine shule, Michael Jackson Shabala (32) na Victoria Ngale Hegira (41) wote wakiwa wafugaji na wakazi wa Sokoine shule.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Oktoba 26, 2026 majira ya saa 15:00 alasiri huko katika eneo la Wami Sokoine picha Kijiji cha Wami Sokoine kata ya Dakawa Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro James Deo Kopilato ambaye bado anatafutwa, akishirikiana na watuhumiwa hao watatu walimtorosha Mwanafunzi huyo.

"Akiwa anatoka shule na wanafunzi wenzake alichukuliwa na kupakiwa kwa nguvu kwenye pikipiki na kisha kutokomea nae kusikojulikana. Aidha, upelelezi wa tukio hili unaendelea ili kumkamata mtuhumiwa aliyebaki na kubaini mahali alipopelekwa Mwanafunzi huyo," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Inadaiwa kuwa kiini cha tukio hilo ni mila potofu za kabila la Kimasai ambao wanaamini kuwa binti akikataa kuozeshwa kwa hiari anachukuliwa kwa nguvu na kisha familia zinakaa na kupatana kwa ajili ya mahari.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.