Skip to main content

MIKONONI MWA POLISI KWA KUKUTWA NA NOTI BANDIA ZA LAKI 8.5 KIGOMA

Na Faustine Kasala - Kigoma.

MIKONONI MWA POLISI KWA KUKUTWA NA NOTI BANDIA ZA LAKI 8.5 KIGOMA
Studio Narration JAMBO FM

MIKONONI MWA POLISI KWA KUKUTWA NA NOTI BANDIA ZA LAKI 8.5 K...

0:00 --:--

Na Faustine Kasala - Kigoma.

Mtuhumiwa mmoja amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma akiwa na Noti bandia 85 za Sh 10,000 kila moja sawa na Shl 850,000 kufuatia Misako na Oparasheni mbalimbali zenye lengo la kubaini na kuzuia uhalifu zinazoendelea kufanywa na Jeshi hilo katika wilaya zote za mkoa wa Kigoma.

Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari May 18/2026 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma Filemon Makungu amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kijiji cha Mwakizega Halmashauri ya wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma akiwa katika harakati za kuziweka pesa hizo kwa wakala wa miamala ya fedha ya mitandao ya simu.

''Katika Oparasheni hiyo April 20,2026 huko katika kijiji cha mwakizega wilaya ya Uvinza Askari Polisi wakiwa katika Doria walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja akiwa na Noti Bandia 85 za Shl 10,000 akifanya utapeli kwa wakala wa miamala ya fedha akijaribu kuweka Noti hizo kwenye mtandao wa Simu, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika,'' aliongeza Kamanda.

Aidha Makungu amesema Askari Polisi kwa kushirikiana na Askari kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania (TAWA) wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja katika kijiji cha Rungwempya wilaya ya Kasulu akiwa na nyara za Serikali vipande vitano vya meno yadhaniwayo kuwa ni ya Tembo.

Watuhumiwa wengine wanne wamekamatwa kufuatia Misako na Oparasheni hiyo wakiwa na pikipiki Tano zidhaniwazo kuwa ni mali ya wizi, watuhumiwa 24 wakiwa na Pombe ya Moshi lita 198 na mitambo Mitano ya kutengenezea pombe hiyo, Pombe zilizopigwa marufuku kuingia nchini aina ya Warangi chupa 200 dawa za kulevya aina ya bangi gunia Sita.

''Katika kudhibiti dawa za kulevya May 13,2026 katika kijiji cha Magarama wilayani Kibondo tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na pikipiki Tatu wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Bangi magunia Matatu, Pia May 17 2026 katika kijiji cha Ilagala Wilayani Uvinza tumemkamata mtuhumiwa mmoja akisafirisha Bangi kwenye Gari la Abiria akiwa ameihifadhi kwenye mabegi Matatu,'' alisema Kamanda Makungu.

Katika hatua nyingine Makungu amesema washitakiwa wawili wa ubakaji na ulawiti wamehukumi vifungo mbalimbali ambapo Mahakama ya wilaya ya Kasulu imemhukumu kifungo cha kwenda Jela miaka 30 mshitakiwa Nuru Hamimu Omary (48) Mganga wa tiba asili mkazi wa kijiji cha Mwamgongo Wilayani Kigoma baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kubaka.

Mshitakiwa mwingine ni Baraka Alphonce (19) Mkulima mkazi wa mtaa wa Kigamboni wilayani Kasulu ambaye naye amehukumiwa kifungo cha kwenda Jela Maisha baada ya Mahakama hiyo kumtia hatiani kwa kosa la kulawiti.

Kamanda Makungu amesisitiza ushiriki wa dhati wa wananchi katika suala zima la kuzuia na kubaini uhalifu na wahalifu kwa lengo la kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.