Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Serikali mkoani Shinyanga, imeanza mkakati wa uongezaji wa madarasa pamoja na matundu ya vyoo katika shule za sekondari, ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2028, kufuatia mtaala mpya wa elimu ambapo elimu ya msingi itakuwa darasa a kwanza hadi la sita tofauti na sasa ambapo elimu hiyo inatekelezwa kwa miaka saba hali itakayopelekea madarasa mawili kumaliza elimu ya msingi kwa pamoja.
Akizungumza leo katika katika kikao kazi cha maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi hao kwa mwaka 2028 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita amewataka wadau wa elimu mkoani humo kushirikiana na serikali kuhakikisha miundo mbinu ya kuwahudumia wanafunzi hao inakamilika kwa wakati kwani kutakuwa na idadi kubwa sana ya wanafunzi watakaotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Amesema, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa elimu katika mkoa huo,hawana budi kuanza maandalizi ya mapema, ili ifikapo mwaka huo 2028 wanafunzi hao watakapohitimu elimu hiyo ya msingi wasikutane na changamoto yeyote ya upungufu wa madarasa,madawati au matundu ya vyoo.
Akizungumzia mtaala mpya, Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Mwl. Samson Hango amesema kuanzia sasa wanafunzi waliopo darasa la tano wanaendelea na mtaala mpya isipokuwa waliopo darasa la sita na la saba wataendelea na mtaala wa zamani wa miaka saba.

Ameongeza kuwa, kufuatia umri lengwa wa madarasa mawili kuanza kidato cha kwanza kwa mwaka huo 2028 hali inayopelekea kuwepo na mahitaji muhimu ya lazima ikiwemo miundo mbinu na rasilimali watu yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili kuweza kuwapokea wanafunzi hao katika shule za sekondari mkoani Shinyanga.
Akielezea Takwimu za mahitaji kwa madarasa hayo mawili yatakayohitimu elimu ya msingi Mwl. Hango amesema kwa mwaka huo kutakuwa na wanafunzi 1,06260 wanaotarajiwa kuanza kidato kwa kwanza huku madarasa 4441 yakihitajika wakati madarasa yaliyopo ni 1419 hali inayopelekea mkoa huo kuwa na mapungufu ya madarasa 1044.

Akielezea mchanganuo wa mapungufu madarasa hayo ki mkoa mwalimu Hango ameainisha kuwa Kahama manispaa kuna maungufu ya madarasa 354 huku Kishapu kukiwa na mapungufu ya madarasa 139.
Msalala kukiwa na mapungufu ya madarasa 166 na wilaya ya Shinyanga ikiwa na pamungufu 132 ambapo manispaa ya Shinyanga ina mapungufu 101 na halimashauri ya Ushetu ikiwa na mapungufu ya 146.

Nao baadhi ya wadau wa elimu waliodhuria kikao hicho akiwemo Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Salum Kitumbo amesema mkakati walionao katika kukabiliana na upungufu huo ni kuwafikia wadau wa maendeleo waliopo katika manispaa hiyo ikiwemo kampuni ya jambo group ili kushirikiana kwa pamoja kumaliza kabisa mapungufu hayo.

Discussion
Reader comments
0 contributions