SINGIDA
Miili ya askari Polisi watano waliofariki dunia Sept 21,2026 katika ajali iliyohusisha gari la Polisi baada ya kugongana na lori la mafuta eneo la Mlima Sekenke Wilaya ya Iramba Mkoani Singida imeagwa leo Jumanne Septemba 22,2026 katika viwanja vya Shule ya Msingi Shelui.
Mkuu wa Mkoa huo Halima Dendego akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ameongoza waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa askari hao ambao walifariki wakati wakitekeleza majukumu yao.
Askari waliofariki katika ajali hiyo ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Shelui, SP Frank Lazima Mwasapili, S/SGT Ussi Hassan, SGT Paulo Silivin Gabriel, PC Ashraf Salumu Kheri na PC Nangida Ramadhani Mushi na walikuwa wakihudumu katika Kituo cha Polisi Shelui.
Mbali na askari hao watano, watu wengine saba ambao walikuwa Mahabusu,walifariki dunia katika ajali hiyo na kusabaisha majeruhi wawili ambao ni dereva wa lori na mhabusu mmoja ambao wanaendelea na matibabu.
Discussion
Reader comments
0 contributions