Skip to main content

MGONTO ATAKA MAISHA YA MZEE WA MIAKA 104 YAIGWE, ASHIRIKI KUMPUMZISHA

Na Saulo Stephen - Singida.

MGONTO ATAKA MAISHA YA MZEE WA MIAKA 104 YAIGWE, ASHIRIKI KUMPUMZISHA

Na Saulo Stephen - Singida.

Mbunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki, Thomas Mgonto ameshiriki Ibada ya Mazishi ya Marehemu Mzee Charles Bulali, mkazi wa kijiji cha Dung’unyi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, ambapo amewaomba wananchi kuenzi na kuiga mfano wa maisha mema aliyoyaishi marehemu wakati wa uhai wake.

Ibada hiyo ya mazishi imefanyika Machi 14, 2026 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mt. Patrisi Dung’unyi, na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi mbalimbali waliokusanyika kumuaga mpendwa wao aliyefariki dunia Machi 11, 2026 baada ya kuugua.

Akizungumza katika ibada hiyo, Mbunge Mgonto ametoa salamu za pole kwa familia ya marehemu na kuwataka kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Amesema kuwa maisha ya Mzee Charles Bulali yameacha historia kubwa ya wema, upendo na mshikamano katika jamii.

Mgonto ameeleza kuwa marehemu alikuwa mtu mkarimu, mcha Mungu na mwenye kujali watu wote bila ubaguzi, jambo lililomfanya kupendwa na kuheshimiwa na jamii iliyomzunguka. Amesisitiza kuwa sifa hizo ni hazina muhimu ambazo jamii inapaswa kuzichukua na kuziendeleza.

Aidha, Mbunge huyo amebainisha kuwa yeye ni miongoni mwa wanafamilia waliopata malezi na ushauri kutoka kwa marehemu, akieleza kuwa mchango wa Mzee Bulali katika malezi na maadili kwa vijana na jamii kwa ujumla ulikuwa mkubwa.

Marehemu Mzee Charles Bulali alizaliwa mwaka 1922 na amefariki akiwa na umri wa miaka 104, akiacha kumbukumbu ya maisha ya hekima, upendo na mshikamano ambayo yataendelea kukumbukwa na jamii ya Dung’unyi pamoja na Wilaya ya Ikungi kwa ujumla.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.