Kufuatia vuguvugu la mgomo wa Madereva katika baadhi ya maeneo nchini, Jeshi la Polisi limeonya mtu au kikundi kinachojihusisha na vitendo vya kuzuia mabasi na malori kuendelea na safari.
Onyo hilo limetolewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania (CP), Awadh Juma hii leo Septemba 29, 2026, jijini Dar es Salaam akidai kuwa vitendo hivyo ni kosa kisheria.
Amesema, "Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali sana kwa mtu yeyote yule atakayebainika kuzuia gari. siyo kuzuia tu, hata kufanya kitu chochote ambacho ni kinyume cha sheria."

Kuhusu taarifa mfumo wa alama (pointi) za leseni, CP Awadh amesema bado haujaanza kutumika na kwamba Wananchi na Madereva wasiongozwe na propaganda za mitandaoni.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi limedqi kiwa linaendelea kufuatilia na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote anayeingilia shughuli za usafirishaji.
Discussion
Reader comments
0 contributions