Mgogoro wa ardhi ambao unahusisha mipaka ya shamba, umesababisha Mwalimu wa Shule ya Msingi Mwongozo, Hidaya Chiwembi (51), kuuawa kikatili katika Kijiji cha Mdenga, kilichopo Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Issa Suleimani amethibisha kutokea kwa tukio hilo la Machi 28, 2026, ambapo marehemu anadaiwa kupigwa kichwani kisha kunyongwa akiwa shambani kwake.
Kamanda Suleimani amesema chanzo kikuu cha mauaji hayo ni mgogoro wa ardhi, huku mtuhumiwa ambaye ametoroka akiendelea kusakwa ili kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Discussion
Reader comments
0 contributions