Skip to main content

MGOGORO WA KIFAMILIA WALETA MADHARA BUNDA, MMOJA ALAZWA

Na Adam Msafiri - Mara.

MGOGORO WA KIFAMILIA WALETA MADHARA BUNDA, MMOJA ALAZWA

Na Adam Msafiri - Mara.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 43, Mkami Maseke, mkazi wa kijiji cha Kurusaga wilayani Bunda mkoani Mara, amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Musoma akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa mikononi kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali katika tukio linalodaiwa kuhusishwa na migogoro ya kifamilia.

Akizungumza akiwa hospitalini, Mkami alidai kuwa tukio hilo lilitokea alipokuwa akifanya shughuli zake shambani, ambapo anamtuhumu aliyekuwa mume wake, Nyamwaga Warioba, kumfuata na kumshambulia. Amesema wawili hao walikuwa wameachana kwa muda kufuatia migogoro ya muda mrefu ya kifamilia, huku taratibu za kurejesha mahari zikiwa tayari zimekamilika.

Mkami ameiambia Tovuti hii kuwa,katika kipindi chote cha maisha yao ya ndoa kulikuwa na migogoro ya mara kwa mara iliyohusisha vipigo na matusi, hali iliyomlazimu kuondoka nyumbani na kurejea kwao kwa ajili ya usalama wake.

Ndugu wa majeruhi, Gunuli Julius, pamoja na mkazi wa kijiji cha Kurusaga, Safri Ndege, walilaani tukio hilo na kuwataka wahusika wa vitendo vya ukatili kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa sasa, Mkami anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere. Ambapo Daktari kutoka kitengo cha mifupa hospitalini hapo, Dkt. Elias Nguti, amesema madaktari wanaendelea kufuatilia hali yake huku akipatiwa huduma stahiki za matibabu.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara kupitia kwa Kamanda wa Polisi mkoa,Pius Lutumo amesema wanaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa anayehusishwa na tukio hilo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.