Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), limerejesha mfumo wa kuandaa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kila baada ya miaka miwili.
Kamati ya utendaji ya CAF (EXCO), ndiyo iliyoridhia uamuzi huo na kwa kurejesha utaratibu uliokuwa ukitumika awali, kabla ya pendekezo la kubadilisha michuano hiyo la kutaka ifanyike kila baada ya miaka minne.

Hatua hii inakuja baada ya Rais wa CAF, Patrice Motsepe, kusema kwamba kamati ya tendaji ingepitia upya uamuzi wa awali wa kuandaa AFCON kila baada ya miaka minne, jambo ambalo liliwashtua wengi.
Hata hivyo, CAF imetaja sababu za kubadili msimamo huo kwamba mashindano mapya ya Afrika, yaliyopendekezwa kwa jina la Africa Nations League, kuwa yatahitaji muda.
Discussion
Reader comments
0 contributions