Skip to main content

MESSOS AHIMIZA MIRADI YA ELIMU, AFYA MKALAMA IKAMILIKE KWA WAKATI

Na Saulo Stephen - Singida.

MESSOS AHIMIZA MIRADI YA ELIMU, AFYA MKALAMA IKAMILIKE KWA WAKATI

Na Saulo Stephen - Singida.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Hajjat Asia Messos, amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu na afya inayotekelezwa katika kata za Kinampundu, Mwanga na Nkalankala, yenye thamani ya jumla ya Shilingi 480,195,000.

Ziara hiyo imelenga kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa, inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma bora kwa wananchi wa Wilaya ya Mkalama.

Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba sita vya madarasa, jengo la utawala, matundu 16 ya vyoo na madarasa mawili ya mfano katika Shule ya Msingi Grace Mesaki, ukamilishaji wa vyumba viwili vya maabara katika Shule ya Sekondari Seth Benjamini, pamoja na ukamilishaji wa chumba kimoja cha maabara katika Shule za Sekondari Selenge na Grace Mesaki.

Mkurugenzi huyo pia alikagua ukamilishaji wa Zahanati ya Malaja na ujenzi wa matundu 24 ya vyoo katika Shule ya Msingi Nkalankala, miradi inayotarajiwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya na elimu katika wilaya hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Hajjat Asia Messos aliwataka wasimamizi wa miradi na wakandarasi kuhakikisha kazi zote zinakamilika kwa wakati, zinazingatia ubora unaohitajika na thamani halisi ya fedha, ili wananchi waanze kunufaika na huduma zilizokusudiwa bila kuchelewa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.