Skip to main content

MENEJA WA ZAMANI WA TRA JELA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

Aliyekuwa Meneja wa TRA Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma, Irving Bagasheki (40) amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma kumkuta na hatia ya makosa mawili ya kujihusisha na nyara za serikali isivyo halali, ambazo ni meno mawili ya tembo yenye thamani ya shilingi milioni 52.

Hukumu hiyo imetolewa Juni 29, 2026 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma, Aristida Tarimo mbele ya Jopo la Mawakili wa Serikali lililoongozwa na Felix Kwetukia.

Ushahidi uliotolewa mahakamani ulionesha kuwa Bagasheki (40) alikamatwa Julai 1, 2024 katika eneo la Beria ya Kihomoka, Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma akiwa ndani ya gari la serikali lenye namba za usajili STL 7274 akijaribu kusafirisha meno hayo mawili ya tembo kinyume na sheria za nchi.

Bagasheki pamoja na watuhumiwa wengine watano walifikishwa mahakamani katika kesi namba 4733 ya mwaka 2025 wakikabiliwa na mashtaka ya kupatikana na nyara za Serikali isivyo halali na kujihusisha na nyara hizo.

Hata hivyo, Mahakama iliwachia huru Watuhumiwa wengine watano ambao ni Hosea Bwandu Ntakimulela, Mathias Kimanuka, Daniel Ezekiel Mbwambo, Ngendamenya Kagozi na Majid Husein Bidebe, baada ya kuridhika kuwa ushahidi haukuwa wa kutosha kuwahusisha na makosa hayo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.