Skip to main content

MCHUNGAJI MSIGWA ATANGAZA KUREJEA CHADEMA

Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Peter Msigwa ametangaza kurejea tena Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kukihama na kijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

MCHUNGAJI MSIGWA ATANGAZA KUREJEA CHADEMA
Studio Narration JAMBO FM

MCHUNGAJI MSIGWA ATANGAZA KUREJEA CHADEMA

0:00 --:--

Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Peter Msigwa ametangaza kurejea tena Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kukihama na kijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Msigwa ametangaza uamuzi huo kupitia andiko lake la Instagram, akisema uamuzi huo umetokana na tafakuri ya kina kuhusu matukio ya ukiukwaji wa haki, utu pamoja na dhuluma dhidi ya uhai wa Binadamu.

Mchungaji Peter Msigwa.

“Kwa dhamira yangu binafsi leo nimejiondoa rasmi kutoka CCM na kurejea CHADEMA kwa kufuata taratibu zote za CHADEMA na Watanzania wote pamoja na wanachama wa CHADEMA,"

"walioumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wangu wa awali naomba radhi kwa dhati pale nilipokuwa kinyume na matarajio yetu ya pamoja katika safari ya kutafuta haki, utu na demokrasia ya kweli,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.