Skip to main content

MBUNGE MGONTO 'AWANOA' HISABATI WANAFUNZI KIDATO CHA NNE IKUNGI SEKONDARI

Na Saulo Stephen - Singida.

MBUNGE MGONTO 'AWANOA' HISABATI WANAFUNZI KIDATO CHA NNE IKUNGI SEKONDARI

Na Saulo Stephen - Singida.

Mbunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki, Thomas Mgonto, ameendelea kuonyesha dhamira yake ya kuinua kiwango cha elimu kwa kuwajengea uwezo wanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Ikungi kupitia ufundishaji wa somo la Hisabati.

Akiwa darasani na wanafunzi, Mgonto aliwafundisha mbinu mbalimbali za kutatua maswali ya Hisabati huku akiwahimiza kujenga nidhamu ya kujisomea, kufanya mazoezi ya kutosha na kujiamini wanapojiandaa na mitihani ya taifa. Alisisitiza kuwa ufaulu mzuri katika Hisabati unafungua fursa nyingi za masomo na taaluma za baadaye.

Hatua hiyo ni sehemu ya kampeni yake ya kutembelea shule mbalimbali ndani ya Jimbo la Ikungi Mashariki kwa lengo la kuongeza hamasa ya wanafunzi katika masomo ya sayansi, hususan Hisabati, na kuboresha matokeo ya kitaaluma.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.