Skip to main content

MBUNGE KIARATU ATAKA UMOJA, MSHIKAMANO KATIKA KUWATUMIKIA WANANCHI

Na Saulo Stephen - Singida.

MBUNGE KIARATU ATAKA UMOJA, MSHIKAMANO KATIKA KUWATUMIKIA WANANCHI

Na Saulo Stephen - Singida.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Yagi Kiaratu, amewataka viongozi wa matawi 65 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuendelea kudumisha umoja na ushirikiano katika kuwatumikia wananchi, kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazoendelea nchini pamoja na kuhamasisha amani na ushiriki wa wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kiaratu ametoa wito huo wakati wa kikao na viongozi wa matawi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mlade Hall, Chuo cha FDC Singida.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Yagi Kiaratu.

Katika kikao hicho, Mbunge huyo pia amewashukuru viongozi hao kwa mchango wao mkubwa uliowezesha ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akieleza kuwa mafanikio hayo yalitokana na umoja, mshikamano na kazi kubwa iliyofanywa na viongozi wa chama kuanzia ngazi ya matawi hadi wilaya.

Amesema viongozi wa CCM walionesha kujituma katika kuhamasisha wananchi, kusimamia shughuli za chama na kuhakikisha sera pamoja na ilani ya CCM zinawafikia wananchi, jambo ambalo lilichangia chama kupata ushindi katika Jimbo la Singida Mjini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.