Skip to main content

MBUNGE KAFITI AAHIDI KUSUKUMA AJENDA SHERIA YA KULINDA TAALUMA MAENDELEO YA JAMII

Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Kafiti William Kafiti, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, amemwakilisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hawa Mchafu, katika Kongamano na Mkutano Mkuu wa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii unaoendelea jijini Mwanza.

Akitoa salamu kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kafiti amesema sekta ya maendeleo ya jamii ina nafasi muhimu katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, akiwataka wataalamu wa fani hiyo kujivunia taaluma yao kwa kuwa ndiyo msingi wa maendeleo endelevu ya taifa.

"Ndugu zangu, maendeleo ya jamii ndiyo msingi mkubwa wa maendeleo ya taifa letu. Ukiangalia hata Dira ya Taifa ya 2050, inahitaji mchango mkubwa wa wataalamu wa maendeleo ya jamii," 

Katika hatua nyingine, Mbunge huyo ameahidi kuendelea kusukuma ajenda ya kuikuza na kuiheshimisha taaluma ya maendeleo ya jamii nchini kwa kuwasilisha pendekezo bungeni la kutungwa kwa sheria mahsusi itakayowezesha kuanzishwa kwa Bodi ya Maendeleo ya Jamii.

Amesema, bodi hiyo itakuwa na jukumu la kusimamia taaluma hiyo, kulinda maslahi ya wataalamu wake pamoja na kurahisisha upatikanaji wa fursa za ajira katika taasisi mbalimbali za umma na binafsi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.