Skip to main content

AZZA AKABIDHI GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KITUO CHA AFYA TINDE

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

AZZA  AKABIDHI GARI LA KUBEBEA WAGONJWA KITUO CHA AFYA TINDE

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad amekabidhi gari jipya la kubebea  wagonjwa (AMBULACE)  kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Kalekwa Kasanga ambalo limetolewa na Serikali kwa ajili ya Kituo cha Afya Tinde.

Akizungumza mbele ya wananchi na viongozi mbalimbali, Mbunge huyo amesema anaifahamu vizuri Tinde na changamoto zinazowakabili wananchi wake, hivyo ataendelea kuzifikisha kero mbalimbali katika mamlaka husika, ili zipatiwe ufumbuzi.

"Niliwaambia matatizo ya wananchi wa Tinde na Jimbo la Itwangi kwa ujumla nayafahamu, najua majukumu yangu. Kuwatekelezea maendeleo wananchi si lazima uwe na fedha mfukoni, bali uwe na uwezo wa kusimama na kubeba matatizo yao," amesema Azza

Aidha, Azza pia amesema ni matokeo ya juhudi za muda mrefu za kuwasilisha mahitaji ya wananchi bungeni, akieleza kuwa Kituo cha Afya Tinde kilikuwa kimekaa kwa takribani miaka mitano bila gari la wagonjwa baada ya ambulance ya awali kupata ajali iliyosababisha kifo cha dereva.

Amekumbusha kuwa hata alipokuwa Mbunge wa Viti Maalum aliomba magari ya wagonjwa kwa ajili ya Tinde na maeneo mengine na kuyakabidhi, lakini baada ya moja ya magari hayo kupata ajali wananchi walibaki bila huduma hiyo muhimu Tinde.

"Mimi sina fedha za kununua ambulance, lakini nina uwezo wa kusimama Bungeni na kushawishi ili wananchi wangu wapate huduma wanazostahili. Leo Serikali imesikia kilio cha wananchi wa Tinde na gari hili limepatikana," amesema.

Mbunge huyo amewataka viongozi wa halmashauri kuhakikisha ambulance hiyo inatunzwa vizuri, iwe na sehemu salama ya maegesho na itumike kwa kuzingatia taratibu, huku akisisitiza kuwa makundi yanayostahili kupata huduma bila malipo yazingatiwe kwa mujibu wa sera za Serikali.

Amesema Kituo cha Afya Tinde kinahudumia idadi kubwa ya wananchi, ambapo kwa mwezi hupokea wagonjwa wa nje kati ya 700 hadi 1,000 na kinahudumia wajawazito wanaojifungua kati ya 200 hadi 250, jambo linalodhihirisha umuhimu wa kupatikana kwa ambulance hiyo mpya.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Tinde, Evance Munisi, amesema kituo hicho kinatoa huduma kwa wananchi wengi lakini bado kinakabiliwa na changamoto za ukosefu wa uzio, wodi za kutosha, mashine ya X-Ray pamoja na nyumba za watumishi.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Dkt. Kalekwa Kasanga, ameishukuru Ofisi ya Rais – TAMISEMI pamoja na Mbunge wa Jimbo la Itwangi kwa juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.