Skip to main content

MBUNGE AGNESS AUNGA MKONO UJENZI WA MADRASA MSIKITI WA QADRIA MUSOMA

Na Adam Msafiri - Mara.

MBUNGE AGNESS AUNGA MKONO UJENZI WA MADRASA MSIKITI WA QADRIA MUSOMA

Na Adam Msafiri - Mara.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Agness Marwa, amekabidhi mifuko 70 ya saruji pamoja na na kiasi cha shilingi milioni 1 taslimu kwa lengo la kuunga mkono  maendeleo ya ujenzi wa madrasa katika Msikiti wa Qadria uliopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Wakizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, viongozi wa msikiti huo wamesema mchango huo utasaidia kuharakisha ujenzi wa madrasa na kuwawezesha vijana kupata mafunzo ya dini yatakayowajengea maadili mema na kuwakinga dhidi ya vitendo visivyofaa katika jamii.

Katibu wa Msikiti wa Qadria, Mohamed Hussin, amesema taasisi za dini zina mchango mkubwa katika malezi ya vijana na kwamba kukamilika kwa madrasa hiyo kutasaidia kuimarisha mafunzo ya dini kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Msikiti wa Qadria, Suleiman Kiraba, amesisitiza umuhimu wa jamii kushiriki katika maendeleo ya taasisi za dini kutokana na mchango wake katika kujenga maadili na mshikamano wa kijamii.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Mbunge Agness Marwa amewataka Watanzania kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na kuheshimiana bila kujali tofauti za makabila au dini. Pia amesisitiza umuhimu wa malezi bora ya vijana kupitia taasisi za dini ili kuwajenga katika misingi ya maadili mema na uzalendo.

Marwa amesema maendeleo ya jamii yanahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali, huku akiahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazolenga kuboresha huduma za kijamii na maendeleo ya wananchi katika Mkoa wa Mara.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.