Skip to main content

MBULU WAADHIMISHA MUUNGANO KWA KUTOA MISAADA HOSPITALI

Na Afarah Suleiman, Mbulu – Manyara.

MBULU WAADHIMISHA MUUNGANO KWA KUTOA MISAADA HOSPITALI
Studio Narration JAMBO FM

MBULU WAADHIMISHA MUUNGANO KWA KUTOA MISAADA HOSPITALI

0:00 --:--

Na Afarah Suleiman, Mbulu – Manyara.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael Semindu ameongoza watumishi wa umma, wanafunzi pamoja na wananchi,wilayani humo,katika kuadhimisha miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo upandaji wa miti pamoja na michezo.

Maadhimisho hayo yalianza kwa zoezi la jogging lililowashirikisha viongozi na wananchi, likifuatiwa na zoezi la upandaji miti katika Shule ya Sekondari Issale. Aidha, washiriki walishiriki katika shughuli ya usafi katika Soko la Mjini Mbulu, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha usafi na utunzaji wa mazingira.

Katika kuendeleza mshikamano na umoja kwenye jamii, walitembelea wagonjwa katika Hospitali ya Mji Mbulu, kwa lengo la kuwafariji wagonjwa ,na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo taulo za kike, mafuta ya kupaka, sabuni za miche na sabuni za unga pamoja na mabeseni.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.