Skip to main content

MAWADATI 500 KUGAWIWA KATIKA SHULE 10 BARIADI VIJIJINI

Na Saada Almasi, Bariadi - Simiyu.

MAWADATI 500 KUGAWIWA KATIKA SHULE 10 BARIADI VIJIJINI

Na Saada Almasi, Bariadi - Simiyu.

Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, imetengeneza Madawati 500 ambayo yanatarajiwa kugawiwa katika shule za sekondari 10 za wilaya hiyo ili kukabiliana na uhaba wa yenzo hiyo muhimu shuleni.Madawati hayo yenye thamani ya shilingi milioni 41 yametengenezwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Hatua hiyo, inafuata baada ya serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kubadili mtaala wake kwa shule zote nchini ikiwepo shule za msingi ambapo kuanzia mwaka 2027 elimu ya msingi itaishia darasa la sita na watoto ambao watakuwa daarasa hilo watafanya mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu hiyo na kujiunga na elimu ya sekondari kidato cha kwanza 2028.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mayala Lucas Shiminji amekiambia kituo hiki kuwa lengo la matengenezo hayo ni kujiandaa kukutana na watoto wengi ambao watahitimu elimu hiyo hivyo ili wasije kukosa nyenzo hiyo maandalizi ya kwapokea ni muhimu kufanyika.

“Kumaliza madarasa mawili kwa wakati mmoja si kitu rahisi hii inaonyesha kutakuwa na wanafunzi wengi baada ya kuhitimu 2027 mahitaji ya madawati na madarasa yatakuwa makubwa sana na moja kati ya vitu ambavyo vitamfanya mwanafunzi akose kusoma vizuri ni uhaba wa madawati na ndiyo maana tunaiunga mkono serkali kwa kupitia mapato yetu ya ndani ya Halmashauri kuweka miundombinu salama kwa watoto,” ameongea Mayala.

Amesema, ”kunapokuwa na mabadiliko ya jambo fulani lazima athari zitatokee na hapa sisi kama Halmashauri tunajiandaa na hayo mabadiliko bila kuiachia serikali peke yake utaona kuna maeneo pia ambayo tumejenga madarasa ni kwa kupitia mapato yetu ya ndani kama tulivyofanya kwa haya madawati na nimatarajio yetu kuwa hakutokuwa na mwanafunzi ambaye atakosa darasa wala dawati katika halmashauri yetu.”

Katika shule 10 ambazo zitapokea madawati hayo, kila shule itakabidhiwa madawati 50 huku mikakati zaidi ya Halmashauri ikiwa ni kuendelea kuboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.