Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limemfikisha mahakamani mshtakiwa wa tatu, Benson John (19), mlinzi (Baunsa), mkazi wa Nyakabungo, Kata ya Isamilo wilayani Nyamagana na kumuunganisha katika kesi ya mauaji ya mkazi wa Mwanza, Mzafuru Faisal Yunusu.
Mzafuru anadaiwa kuuawa kwa kipigo katika baa ya Las Vegas iliyopo eneo la Kona ya Bwiru, mtaa wa Nyamanoro, wilaya ya Ilemela baada ya kushindwa kulipa bili ya shilingi 8000.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Mwanahawa Changale, kuwasilisha ombi mahakamani hapo la kutaka hati mpya ya mashtaka inayomwongeza mtuhumiwa huyo ipokelewe chini ya kifungu cha 251 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023.
Wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa. Kufuatia marekebisho hayo ya hati ya mashtaka katika shauri la jinai namba 10492 la mwaka 2026, idadi ya washtakiwa wanaokabiliwa na kesi h
Discussion
Reader comments
0 contributions