Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la saba kwa Wanafunzi wahitimu wa 2026.
Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Saidi Ally Mohamed akitangaza matokeo hayo amesema, watahiniwa 970,876 wamefaulu kwa madaraja ya A, B na C sawa na asilimia 85.22 kati ya watahiniwa 1,139,273 waliofanya mtihani.
Watahiniwa 31 wamefutiwa matokeo ya mitihani hiyo, ambapo kati ya watahiniwa 31 waliofutiwa matokeo ya mitihani, 26 wamefutiwa kutokana na udanganyifu na watano wamefutiwa kwa kuandika matusi.

DONDOO MUHIMU:
- Kiwango cha Ufaulu: Jumla ya watahiniwa 970,876 (asilimia 85.22) wamefaulu katika madaraja ya A, B na C kati ya watahiniwa 1,139,273 waliofanya mtihani huo.
- Wavulana na Wasichana: Wavulana walipata ufaulu wa asilimia 86.18, huku wasichana wakiwa na asilimia 84.43 (ingawa idadi ya wasichana waliofaulu jumla ni 527,622 dhidi ya wavulana 443,254).
- Waliofutiwa Matokeo: Watahiniwa 31 wamefutiwa matokeo yao (26 kwa udanganyifu na 5 kwa kuandika matusi).
kuona matokeo yote tazama link hapa chini.👇👇👇👇
https://matokeo.necta.go.tz/results/2026/psle/results/shl_ps0204166.htm
Discussion
Reader comments
0 contributions