Skip to main content

MARUFUKU WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA, VIJIJI KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA VIWANJA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

MARUFUKU WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA, VIJIJI KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA VIWANJA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Manispaa ya kahama mkoani shinyanga, imepiga marufuku kwa wenyeviti wa seerikali za mitaa na vijiji kujihusisha na mikataba ya mauziano ya viwanja na maeneo kwakuwa ni kinyume na utaratibu wa sheria za manispaa.

Agizo hilo limetolewa na kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama  Steven Magala wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha ndani cha wenyeviti hao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa manispaa hiyo.

“Mwenyekiti ana majukumu yake kisheria na jukumu lake kubwa ni kufanya utambuzi wa mkazi wa eneo husika,na haruhisiwi kushuhudia mauziano ya kiwanja au eneo lolote katika manispaa ya Kahama kazi ya mwenyekiti ni kutambua eneo la muuzaji katika eneo lake” Amesema Magala.

Sambamba na hayo Magala amewataka wananchi wanaohitaji kununua kiwanja wafike katika ofisi za ardhi manispaa ya Kahama ili kufuatilia kama eneo lipo halali a halina pingamizi lolote mahakamani au mgogoro wa mume na Mke” Ameongeza Magala.

Magala amesema kuwa Manispaa ya Kahama imekuwa na migogoro mingi ya ardhi ambayo mingi ya migogoro hiyo inasababishwa na wenyeviti wa mitaa kushuhudia uuzaji wa viwanja mara mbili kwa watu wawili tofauti na wengine kushirikiana na wanunuzi wasio waamiifu.

“Kahama imekuwa na migogoro mingi ya ardhi,na hali hii inasababishwa na baadhi ya wenyeviti kushuhudia mauziano mara mbili kwa watu wawili tofauti na wenyeviti wengine kushirikiana na wanunuzi ambao siyo waaminifu” Ameongeza Magala.

Nao baadhi  ya wananchi wa Manispaa ya Kahama wameipongeza manispaa ya Kahama kwa uamuzi huo na kwamba hali hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa wananchi hususan wanawake wajane ambao wanatapeliwa vwanja na nyumba zao mara kwa mara.

“Kwakweli uamuzi huu ni mzuri sana katika manispaa yetu itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi baina ya wananchi hasa kwa wajane,Mana wajane wamezulumika maeneo yao kupitia hawa hawa wenyeviti wa mitaa” Amesema Mariam Yasin na Mzee Solomoni Hassan wakazi wa mtaa wa Igomelo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.