Skip to main content

MARUFUKU UBEBAJI HOLELA WA MIZIGO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewakamata madereva 72 wa Pikipiki za mizigo maarufu kama Guta kwa kupakia mizigo kwa namna inayohatarisha usalama barabarani, na kutoa onyo kali baada ya kubainika baadhi yao wamekuwa wakihatarisha maisha ya watumiaji wengine wa barabara.

MARUFUKU UBEBAJI HOLELA WA MIZIGO
Studio Narration JAMBO FM

MARUFUKU UBEBAJI HOLELA WA MIZIGO

0:00 --:--

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewakamata madereva 72 wa Pikipiki za mizigo maarufu kama Guta kwa kupakia mizigo kwa namna inayohatarisha usalama barabarani, na kutoa onyo kali baada ya kubainika baadhi yao wamekuwa wakihatarisha maisha ya watumiaji wengine wa barabara.

Akizungumza baada ya kutoa elimu kwa madereva hao, Kamanda wa Polisi wa huo DCP Wilbroad Mutafungwa amesema amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na watumiaji wengine wa barabara kuhusu ukiukwaji wa sheria na taratibu za usalama.

Baadhi ya madereva wa Pikipiki za miguu mitatu maarufu Guta wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilbroad Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa amesema upakiaji wa mizigo inayozidi ukubwa wa chombo ni hatari kwa kuwa barabara hizo hutumiwa na makundi mbalimbali likiwemo la watembea kwa miguu akitolea mfano ajali iliyotokea hivi karibuni ambapo Guta lililobeba Miringoti iliyochomoza nje kuligonga gari na kusababisha dereva kupoteza maisha.

Baadhi ya Pikipiki za miguu mitatu maarufu Guta zilizokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza.

Amesema Jeshi la Polisi limechukua hatua ya kutoa elimu badala ya kuchukua hatua za kisheria na kwamba amemuagiza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza, SSP Sunday Ibrahim kuandaa kikao maalum cha elimu kwa madereva hao siku ya Ijumaa Septemba 25,2026 ili kuwaelimisha madhara ya ukiukwaji wa sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilbroad Mutafungwa akizungumza na madereva wa Pikipiki za miguu mitatu maarufu Guta

Aidha, amewataka madereva hao kutambua kuwa matumizi ya barabara ni haki ya kila mtu na kuwa makini kwa kutazama pande zote wanapokuwa barabarani na kutoa nafasi kwa watumiaji wengine wa barabara ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.