Skip to main content

MARUFUKU BIASHARA YA NGONO TABORA YATANGAZWA KUIKABILI EBOLA

Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mohamed Mtulyakwaku, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Wella ametangaza marufuku ya biashara ya ngono katika Wilaya ya Tabora na maeneo yote yanayoizunguka kama sehemu ya juhudi za kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola.

MARUFUKU BIASHARA YA NGONO TABORA YATANGAZWA KUIKABILI EBOLA

Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mohamed Mtulyakwaku, akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Wella ametangaza marufuku ya biashara ya ngono katika Wilaya ya Tabora na maeneo yote yanayoizunguka kama sehemu ya juhudi za kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Ebola.

Tamko hilo limetolewa wakati wa kikao maalumu cha Kamati ya Afya ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kilicholenga kujadili na kuimarisha mikakati ya kukabiliana na tishio la ugonjwa huo. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Tabora na kuwahusisha viongozi pamoja na wataalamu wa afya.

Akizungumza katika kikao hicho, Mtulyakwaku amesema kuwa Ebola husambazwa kwa njia mbalimbali zinazohusisha mgusano wa karibu wa mwili, ikiwemo kujamiiana, kugusa mtu aliyeambukizwa au kushika vitu vilivyotumiwa na mgonjwa. Kutokana na hali hiyo, ameeleza kuwa biashara ya ngono inaweza kuongeza hatari ya maambukizi na hivyo inapaswa kusitishwa mara moja.

Aidha, amewataka viongozi wa dini kutumia nafasi zao kutoa elimu kwa waumini kuhusu namna ya kujikinga dhidi ya Ebola pamoja na kuhamasisha wananchi kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya. Pia amesisitiza umuhimu wa kuliombea Taifa ili liweze kuvuka salama kipindi hiki cha tahadhari.

Katika hatua nyingine, Mtulyakwaku amemwelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora kushirikiana na timu ya wataalamu walioteuliwa kukabiliana na ugonjwa huo kuhakikisha vifaa tiba vinapatikana kwa wakati katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa watakaobainika kuwa na maambukizi ya Ebola.

Kwa upande wake, Afisa Afya wa Manispaa ya Tabora, Laurent Lushekya, amefafanua kuwa Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha Ebola na huenea kwa urahisi kupitia mgusano wa moja kwa moja na mgonjwa au vitu vilivyoguswa na mgonjwa huyo.

Lushekya amewataka wananchi kuchukua tahadhari zote zinazopendekezwa na wataalamu wa afya, ikiwa ni pamoja na kuepuka kugusa vitu vya mgonjwa wa Ebola, kutokula nyama pori isiyokaguliwa na mamlaka husika, pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.