Serikali ya Marekani, imeijulisha rasmi Afrika Kusini nia yake ya kusitisha hadhi ya nchi hiyo, kama mnufaika wa Sheria ya Ukuaji na Fursa kwa Afrika (AGOA), mpango unaotarajia kuanza Januari 1, 2027.
Hatua hiyo inafuatia utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump kuibua wasiwasi kuhusu Taifa hilo la kusini mwa Afrika kuhusu madai ya Rushwa na hongo, vizuizi vya biashara vinavyoathiri biashara za Marekani na vizuizi vya ufikiaji wa soko la kilimo.
Kingine ni Ulinzi wa uwekezaji na haki miliki, maamuzi ya sera ya mambo ya nje na mahusiano na serikali zinazoonekana na Washington kama tishio kwa usalama wa taifa wa Marekani.

HII INA MAANA GANI KWA AFRIKA KUSINI?
AGOA inazipa nchi zinazostahili za Afrika fursa ya upendeleo ya kuingia katika soko la Marekani. Kupoteza manufaa haya kunaweza kuwa na madhara makubwa kwa wauzaji nje wa Afrika Kusini, biashara, uwekezaji na uwezekano wa maelfu ya ajira.
Hata hivyo, hili ndilo swali kubwa zaidi: Je, sera ya mambo ya nje ya Afrika Kusini inastahili kuhatarisha uhusiano wake wa kiuchumi na moja ya nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani?
Je, Rais Cyril Ramaphosa na serikali yake wanapaswa kufikiria upya mbinu yao kwa Washington kabla ya uamuzi huu kuanza kutumika?
Au Afrika Kusini inapaswa kusimama imara na kukataa kushinikizwa na Marekani?
AFRIKA KUSINI, MAONI YAO NI YAPI?
Maslahi ya nani yanapaswa kuja kwanza: ushirika wa kisiasa au mustakabali wa kiuchumi wa Waafrika Kusini wa kawaida?
Hata hivyo, tishio hilo pia linaikabili Swrikali ya Nchi ya Rwanda, inayoongozwa na Paul Kagame.
Discussion
Reader comments
0 contributions