Serikali ya Marekani, imemuwekea vikwazo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Nchini, Faustine Mafwele kwa madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Vikwazo hivyo vinampiga marufuku Mafwele kuingia Marekani kutokana na matukio ya mateso dhidi ya Wanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi na Agather Atuhaire wa Uganda Mei 2025.

Taarifa kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, inasema mwaka uliopita maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania waliwakamata, kuwatesa, na kuwadhulumu kingono Atuhaire na Mwangi.

Wanaharakati hao wa haki za binadamu walikuwa jijini Dar es Salaam kuhudhuria kesi ya kiongozi wa upinzani na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Discussion
Reader comments
0 contributions