Skip to main content

MAPYA: VIKOSI VYA ETHIOPIA VYAINGIA MPAKANI MWA ERITREA

Vikosi vya jeshi la Ethiopia, vimekita kambi Mji Mkuu wa kimkakati wa Adwa Karibu na Mpaka wa Eritrea.

MAPYA: VIKOSI VYA ETHIOPIA VYAINGIA MPAKANI MWA ERITREA
Studio Narration JAMBO FM

MAPYA: VIKOSI VYA ETHIOPIA VYAINGIA MPAKANI MWA ERITREA

0:00 --:--

Vikosi vya jeshi la Ethiopia, vimekita kambi Mji Mkuu wa kimkakati wa Adwa Karibu na Mpaka wa Eritrea.

Taarifa kutoka eneo la mgogoro zinaeleza kuwa vikosi vya Serikali Kuu ya Ethiopia pamoja na vikosi vilivyo na ukaribu na serikali vimesogea mbele zaidi katika Mkoa wa Tigray, hali inayoelezwa kuamsha hofu ya kuongezeka kwa mzozo mpana zaidi katika eneo hilo la Pembe ya Afrika.

Kulingana na wakazi wa eneo hilo, vikosi vya jeshi wa serikali ya Ethiopia na wanamgambo waliovalia sale na viba uso wakiwa na silaha na magari ya kivita wameonekana wakiingia katika mji wa Adwa, uliopo karibu na mpaka wa nchi jirani ya Eritrea, kufuatia kuondoka kwa waasi wa Tigray.

Wakati huo huo, vikosi vinavyoungwa mkono na serikali vimetwaa tena udhibiti wa mji mkuu wa mkoa huo, Mekelle, baada ya kuibuka tena kwa mapigano mapya dhidi ya Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF).

Hayo yanajiri wakati aliiyewahi kuwa kiongozi wa Tigray, ambaye kwa sasa anahudumu kama mshauri wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed Ali , ameahidi kuwepo kwa "mabadiliko yanayoonekana" katika mkoa huo, ingawa hakutoa maelezo ya kina zaidi kuhusu mabadiliko hayo.

Katika hatua nyingine inayonasibishwa na kurejea kwa utulivu wa muda, Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines limerejesha rasmi safari zake za ndege kuelekea Mekelle kwa mara ya kwanza tangu waasi walipokamata uwanja wa ndege wa mji huo tarehe 23 Septemba. Waasi hao waliondoka uwanjani hapo tarehe 3 Oktoba, na kutoa fursa kwa majeshi ya serikali kuingia mjini humo.

Serikali ya Ethiopia inaishutumu nchi jirani ya Eritrea kwa kuwaunga mkono waasi hao na kutuma wanajeshi wake kuvuka mpaka kuingia nchini Ethiopia. Hata hivyo, Eritrea imekanusha vikali tuhuma hizo na kulitaka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuingilia kati mzozo huo.

Kadharika Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito kwa pande zote zinazohasimiana kusitisha mara moja uhasama badala yake kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kutafuta suluhu ya amani.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.