Hali ya taharuki na sintofahamu imeibuka Nchini Ethiopia kufuatia mauaji ya Watu wasiopungua 60 kuuawa katika mashambulizi yaliyolenga jimbo la Oromia Magharibi mwa Ethiopia.
kulingana na taarifa iliyotolewa na Kanisa la dhehebu la Orthodox la Ethiopia na kuripotiwa na vyombo vya habari nchini humo viongozi wa kidini wamethibitisha kuwa waathiriwa wote wa mashambulizi hayo walikuwa Wakristo, walakini hawakutoa maelezo ya kina kuhusu kundi au watu waliohusika na unyama huo.

Oromia ndilo jimbo kubwa zaidi nchini Ethiopia likiwa na idadi ya watu takriban milioni 40. Eneo hilo limekuwa likikabiliwa na migogoro ya muda mrefu ya makundi ya waasi pamoja na mivutano ya kimbari na kidini kati ya jamii za Waislamu, Waprotestanti, na Wakristo wa Orthodox mivutano inayodaiwa kutumiwa kama kinga dhidi ya makundi ya watu wenye silaha.
Shirika la ufuatiliaji wa migogoro la ACLED (Armed Conflict Location & Event Data Project), shambulio hilo linasadikiwa kuchochewa na chuki za kidini zilizowalenga Wakristo wa Orthodox, huku kukiwa na taarifa za kuporwa kwa kanisa moja la Orthodox eneo hilo.

ACLED imeongeza kuwa mashambulizi dhidi ya Wakristo wa Orthodox katika jimbo hilo yameongezeka tangu Februari 2023 na yamezidi kuwa makali katika mwaka mmoja uliopita.
Hadi sasa, uwezekano wa kuhusika kwa kundi la waasi la Oromo Liberation Front (OLF) kundi kuu la waasi linalofanya operesheni zake jimboni Oromia haujathibitishwa ingawaje kuna utiliwaji shaka wa kuhusika kwake.

Wakati hayo yanajiri Tume ya Haki za Binadamu ya Ethiopia (EHRC), ambayo ni taasisi inayofadhiliwa na serikali inayojiendesha kwa kujitegemea, imeziambia duru kuwa inaendelea "kufuatilia kwa karibu hali hiyo" na "kuchunguza maelezo ya kina" ya mashambulizi hayo.
Shambulio hilo linalotajwa kuwa la kinyama dhidi ya ubinaadamu linafanyika wakati ambapo vutanikuvute imeendelea kuripotiwa baina ya Vikosi vya waasi vya upinzani vinavyonasibishwa na uungwaji mkono wa Serikali ya Eritrea dhidi ya serikali mjini Tigray.
Discussion
Reader comments
0 contributions