Katika hatua za hivi punde Marekani imetangaza utekelezaji wa mpango wake wa kusimika kambi mbili za kijeshi kusini mwa Greenland na kingine pwani ya mashariki mwa eneo hilo.

Duru kutoka Barani Ulaya zinaeleza hayo yanajiri kulingana na mkataba unaotarajiwa kutiwa saini kati ya Marekani na serikali za Denmark pamoja na Greenland katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa unaotarajiwa kufanyika jijini New York siku ya hii leo.
Hata hivyo vyanzo vya karibu vimeweka bayana maeneo yaliyochaguliwa ikiwa ni pamoja na Narsarsuaq eneo ambalo idadi yake ya wakazi imepungua kwa kasi ambapo pia eneo hilo kwa sasa liko chini ya kituo cha kijeshi kinachotumiwa kwa sasa na kikosi maalumu cha mbwa cha jeshi la Denmark (Sirius Dog Sled Patrol).

Sintofahamu imeibuka katika mkataba huo kutokana na maandishi ya mkataba huo kutowekwa bayana kwa umma kutokana na kile ambacho vyanzo hivyo vimedokeza kwa sharti la kutotajwa majina
Serikali za Denmark na Greenland zimearifiwa kutojibu kile mashirika ya habari ya kimataifa yalihoji juu ya makubaliano hayo mapya na yanayotajwa kuzua sintofahamu kutokana na tofauti za hapo kabla baina ya mataifa hayo na Marekani.

Serikali ya Denmark imeeleza kuwa mkataba huo unalenga kuweka usalama wa eneo la Arctic chini ya usimamizi wa Muungano wa Kijeshi wa umoja wa kujihami NATO, badala ya kuliachia eneo hilo mikononi mwa Marekani na Denmark pekee.
Hatua hii inakuja baada ya muda wa takribani miezi 8 ya vuta nikuvute na shinikizo kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye amekuwa akisisitiza nia yake ya kutaka Marekani idhibiti Greenland, na baadae kutengeu dhamira hiyo ya kutumia nguvu za kijeshi na za kiuchumi kutwaa eneo hilo linalojitawala nusu kutoka kwa Denmark.

Tishio hilo la Trump, lililofikia kilele mwezi Januari, lilizua mgogoro wa kidiplomasia ndani ya muungano wa umoja wa kujihami NATO na kuzilazimu Denmark na Greenland kuingia katika mashauriano dhidi ya serikali ya Washington ili kupunguza purukushani hiyo.
Kadharika fukuto limetajwa kusalia juu mapango mpya wa Marekani kutakana na kura za maoni za wakazi wa eneo hilo kukataa vikali mkataba huo.

Sanjari na hayo enzi za Vita Baridi, Marekani ilikuwa na vituo vya kijeshi 17 pamoja na wanajeshi zaidi ya 10,000 nchini Greenland. Kwa sasa, kimesalia kituo kimoja cha anga cha Pituffik Space Base chenye mchangamano na wanajeshi wa Marekani kikiwa na takriban wanajeshi 150 wa Marekani.
Discussion
Reader comments
0 contributions