Skip to main content

MAPOKEZI YA MWENGE KISHAPU: DAS FATMA ATOA HAMASA KWA WANANCHI

Na Eunice Kanumba –Shinyanga.

MAPOKEZI YA MWENGE KISHAPU: DAS FATMA ATOA HAMASA KWA WANANCHI

Na Eunice Kanumba –Shinyanga.  

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Fatma Mohamed, amewahimiza wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru, unaotarajiwa kuwasili wilayani humo Agosti 18, 2026.

DAS Fatma ametoa hamasa hiyo  wakati akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kishapu,  Peter Masindi, katika mazoezi ya  'jogging' yaliyolenga  kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.

Amesema Mwenge wa Uhuru ni alama muhimu ya Taifa inayobeba ujumbe wa amani, umoja, mshikamano na maendeleo, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kuupokea na kushiriki katika shughuli mbalimbali utakapowasili wilayani humo.

Ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya Mwenge 2026 "Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo," wakiongozwa na mkimbiza Mwenge kitaifa Wazo Michael Mwang’onda.

Kila mwaka, Mwenge wa Uhuru huzunguka katika mikoa mbalimbali nchini ukibeba ujumbe unaolenga kuelimisha jamii kuhusu masuala ya maendeleo, afya, elimu, mazingira na kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Wananchi wametakiwa kuendelea kuunga mkono ujumbe wa Mwenge wa Uhuru kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na kutekeleza kwa vitendo maelekezo yanayotolewa kwa manufaa ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.