Skip to main content

MAPENDEKEZO MATANO YA NDEJEMBI KUIMARISHA AMANI MAZIWA MAKUU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ametoa mapendekezo matano kwa nchi za ukanda wa Maziwa Makuu yanayolenga kuimarisha amani, usalama na mshikamano wa kikanda, akisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wanawake katika uongozi na utatuzi wa migogoro.

MAPENDEKEZO MATANO YA NDEJEMBI KUIMARISHA AMANI MAZIWA MAKUU
Studio Narration JAMBO FM

MAPENDEKEZO MATANO YA NDEJEMBI KUIMARISHA AMANI MAZIWA MAKUU

0:00 --:--

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ametoa mapendekezo matano kwa nchi za ukanda wa Maziwa Makuu yanayolenga kuimarisha amani, usalama na mshikamano wa kikanda, akisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wanawake katika uongozi na utatuzi wa migogoro.

Ndejembi ametoa mapendekezo hayo leo Novemba 2, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa wabunge wanawake wa nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema hatua ya kwanza ni kuimarisha ushiriki wa wanawake katika michakato ya kufanya maamuzi kwa kuhakikisha wanapata nafasi katika mabunge, serikali, taasisi za usalama, kamati za amani na mazungumzo ya kutafuta suluhu za migogoro.

Pendekezo la pili ni kuimarisha diplomasia ya wanawake na mifumo ya upatanishi kwa kuendeleza mitandao ya wanawake wapatanishi katika ngazi za jamii, kitaifa na kikanda ili kusaidia kuzuia migogoro na kujenga mawasiliano.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya ukatili, kuboresha huduma kwa waathirika na kuhakikisha wanapata msaada, haki na ulinzi unaostahili.

Pendekezo la nne ni kuwekeza kwa wanawake na vijana kupitia elimu, mafunzo, ujuzi, ujasiriamali na fursa za kiuchumi, huku la tano likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa kikanda na uwajibikaji kwa kuweka mipango madhubuti ya utekelezaji na mifumo ya kufuatilia maendeleo.

Amesema mapendekezo hayo yakitekelezwa yatasaidia kuimarisha amani na usalama katika ukanda wa Maziwa Makuu kwa manufaa ya wananchi wake.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.