Skip to main content

MAPATO: WATENDAJI KATA GEITA WAHIMIZWA UWAJIBIKAJI

Na Ibrahim Rojala - Geita.

MAPATO: WATENDAJI KATA GEITA WAHIMIZWA UWAJIBIKAJI

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Yefred Myenzi amesisitiza uwajibikaji na ufanisi kwa Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Manispaa hiyo katika kazi na ukusanyaji madhubuti wa mapato ya halmashauri hiyo.

Ametoa maagizo hayo kupitia  kikao kazi na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa Manispaa hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa EPZ Bombambili, Manispaa ya Geita Machi 31,2026.

Kupitia kikao hicho, Myenzi ameelezea umuhimu wa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu, akiwataka watendaji kuziba mianya yote inayosababisha upotevu wa mapato ya halmashauri akieleza kuwa jukumu la kuhakikisha wananchi wanazingatia sheria na taratibu za ulipaji kodi liko mikononi mwao.

“Ni wajibu wenu kuhakikisha kila mwananchi anatekeleza wajibu wake wa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria. Hii ndiyo njia ya kuhakikisha maendeleo ya Halmashauri yanapatikana,” amesisitiza Myenzi.

Aidha, amebainisha kuwa kila mwananchi ana haki ya kusikilizwa na kupatiwa ufumbuzi wa changamoto zake na hivyo kuwataka watendaji kuwa karibu na wananchi na kuwahudumia kwa ufanisi na heshima.

Kwa upande wake, Masalu Fulano, akizungumza kwa niaba ya Afisa Lishe wa Manispaa ya Geita, amesema Idara ya Afya kupitia kitengo cha lishe imefanya ziara katika shule mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha walimu na viongozi kutoa elimu kwa wazazi kuhusu umuhimu wa kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni.

Ameeleza kuwa katika ziara hizo, wamekagua mazingira ya uandaaji wa chakula na kuhakikisha yanazingatia usafi na taratibu zote za kiafya, pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya wanafunzi.

Bi. Masalu ametoa wito kwa watendaji wa kata na Mitaa kuendelea kuhamasisha wazazi kushiriki kikamilifu katika mpango wa chakula shuleni, akisisitiza kuwa lishe bora ni msingi muhimu wa maendeleo ya mtoto katika elimu na afya.

Akihitimisha kikao hicho, Mkurugenzi Myenzi amehimiza utunzaji wa mazingira kwa kuendeleza usafi na kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya Manispaa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.