Skip to main content

MANYONI YAFIKIWA UBORESHWAJI MTANDAO WA MAJI, MJITI WASHUSHA PUMZI

Na Saulo Stephen - Singida.

MANYONI YAFIKIWA UBORESHWAJI MTANDAO WA MAJI, MJITI WASHUSHA PUMZI

Na Saulo Stephen - Singida.

Mradi wa ujenzi wa mtandao wa maji wenye thamani ya Shilingi 87,284,483 umezinduliwa katika Kijiji cha Mjiti, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, ukiwa na lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa eneo hilo.

Mradi huo umezinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Ndugu Wazo Mwang'onda, kwa kuweka jiwe la msingi ikiwa ni sehemu ya shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Katika utekelezaji wake, Serikali Kuu imechangia Shilingi 73,784,483, huku wananchi wakichangia nguvu zenye thamani ya Shilingi 13,500,000, jambo linaloonesha ushiriki wao mkubwa katika kuleta maendeleo ya kijiji chao.

Akizungumza baada ya kuzindua mradi huo, Mwang'onda aliwataka wananchi kuutunza mradi huo kwa kuhakikisha miundombinu ya maji inalindwa dhidi ya uharibifu ili huduma hiyo iendelee kudumu na kuwanufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi, huku akiwahimiza wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.