Skip to main content

MANYARA WAADHIMISHA MIAKA 62 YA MUUNGANO KWA KUFANYA SHUGHULI ZA KIJAMII

Na Afarah Suleiman, Babati - Manyara.

MANYARA WAADHIMISHA MIAKA 62 YA MUUNGANO KWA KUFANYA SHUGHULI ZA KIJAMII

Na Afarah Suleiman, Babati - Manyara.

Mkoa wa Manyara umeaadhimisha miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo upandaji wa miti , kufanya usafi katika Halmashauri ya mji wa Babati pamoja na kufanya michezo mbalimbali.

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, mkuu wa wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda amewataka wananchi kuendelea kuimarisha muungano pamoja na amani na mshikamano wa Taifa.

Amesema Taifa la Tanzania limeendelea kuwa mfano wa utulivu wa kisiasa,mshikamano wa kijamii , na maendeleo ya kijamii ambapo yote hayo yamesababishwa na umoja uliwekwa na mwalimu Julias Kambarage Nyerere na shekhe Amani Karume.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Mariam Muhaj amesema, katika kuadhimisha siku hiyo wamepanda miti katika maeneo mbalimbali ya mkoa , kufanya usafi pamoja na mazoezi na kutoa wito kwa jamii kuendelea kutanza mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti katika maeneno yanayo tuzunguka.

Nao baadhi ya Wazee kutoka mkoani Manyara ambao walishuhudia muungano huo mwaka 1964, wamesema wamefurahia uwepo wa muungano kutokana na umoja na amani iliyopo.

Maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar huadhimishwa april 26 kila mwaka, na kwa mkoa wa Manyara maadhimisho hayo yameadhimishwa leo na kauli mbiu ya miaka 62 ya muungano kwa mwaka huu ni amani, umoja na mshikamano ni msingi wa maendeleo endelevu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.