Na Afarah Suleiman, Mbulu - Manyara.
Zaidi ya vijana 600 Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, wameshiriki utoaji mawazo ya ubunifu wa biashara, kwenye kongamano maalumu la Vijana Platform lililoandaliwa na Halmashauri hiyo.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mkuu wa Wlaya ya Mbulu, Michael Semindu amesema Halmashauri imetenga zaidi ya shilingi milioni mia mbili kwa ajilili ya kuwawezesha vijana hao kiuchumi katika kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake afisa vijana Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Edes Melly amesema kupitia kongamano hilo vijana wameanza kunufaika na fursa za uchumi wa kidigitali, kwa kubuni teknolojia mbali mbali zitakazosaidia kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii.
Nao baadhi ya vijana walioshiriki kongamano hilo, wameomba Serikali iwawezeshe kiuchumi ili waweze kujiajiri kupitia ubunifu wao.




Discussion
Reader comments
0 contributions