Skip to main content

MAMA, BABA LISHE WAOMBA ENEO MAALUMU MJI WA SERIKALI MTUMBA

Mama na baba lishe mkoani Dodoma wameiomba Serikali kuwatengea eneo maalumu la kufanyia biashara ya chakula katika Mji wa Serikali Mtumba, wakisema hatua hiyo itawawezesha kunufaika na fursa za kiuchumi zitakazotokana na uwepo wa watumishi, viongozi na wageni.

MAMA, BABA LISHE WAOMBA ENEO MAALUMU MJI WA SERIKALI MTUMBA
Studio Narration JAMBO FM

MAMA, BABA LISHE WAOMBA ENEO MAALUMU MJI WA SERIKALI MTUMBA

0:00 --:--

Mama na baba lishe mkoani Dodoma wameiomba Serikali kuwatengea eneo maalumu la kufanyia biashara ya chakula katika Mji wa Serikali Mtumba, wakisema hatua hiyo itawawezesha kunufaika na fursa za kiuchumi zitakazotokana na uwepo wa watumishi, viongozi na wageni.

Wakizungumza baada ya kutembelea mji huo leo, Alhamisi, Oktoba 29, 2026, siku moja kabla ya uzinduzi wake, wamesema uwekezaji uliofanyika katika ujenzi wa majengo ya Serikali unaweza kufungua fursa kwa wajasiriamali wa sekta ya chakula, iwapo watapewa nafasi ya kuwahudumia watu watakaofika kwa shughuli mbalimbali.

Mwenyekiti wa Mama na Baba Lishe Tanzania, Havijawa Omari, amesema ziara hiyo imewawezesha kujionea maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Serikali na kubaini fursa zinazoweza kuwasaidia kukuza shughuli zao za kiuchumi.

“Mradi huu ni mkubwa, ofisi ni pana na nzuri. Sisi mama lishe tunaona kuna fursa ambapo tunaweza kupata nafasi ya kuwauzia viongozi chakula, na sisi tukapata kipato,” amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baba Lishe, Yahaya Hassan, amesema ziara hiyo imekuwa na manufaa kwao kwa kuwa wamepata fursa ya kutembelea Mji wa Serikali Mtumba na kushiriki semina iliyowapa elimu kuhusu namna ya kuandaa vyakula vya asili.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.