Skip to main content

MAKONDA: WANANCHI TUMIENI FURSA ZA KIUCHUMI KUJIKWAMUA

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza, kuhakikisha wanatumia fursa za kiuchumi zinazowazunguka kufanya shughuli halali kama biashara, ili kukuza uchumi wao wa kila siku.

MAKONDA: WANANCHI TUMIENI FURSA ZA KIUCHUMI KUJIKWAMUA
Studio Narration JAMBO FM

MAKONDA: WANANCHI TUMIENI FURSA ZA KIUCHUMI KUJIKWAMUA

0:00 --:--

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza, kuhakikisha wanatumia fursa za kiuchumi zinazowazunguka kufanya shughuli halali kama biashara, ili kukuza uchumi wao wa kila siku.

Makonda ameyasema hayo Oktoba 12, 2026 wilayani Nyamagana wakati akikagua mradi wa Ujenzi, Upanuzi na Uboreshaji wa Bandari ya Mwanza Kaskazini unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 18.606 ikijumuisha VAT.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Waziri Makonda amesema “Lazima mwananchi abadilishe mtazamo kwanza ndani yake awe na kiu ya kutafuta kipato chake wakati serikali nayo ikiendelea kuboresha miundombinu katika kuhakikisha inatoa huduma bora za maji, afya, elimu na barabara.”

Aidha, alisisitiza kuwa amani ni msingi wa utaifa na nguzo ya maendeleo, hivyo kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake katika kulinda amani na umoja kwenye jamii na taifa kwa ujumla.

Waziri Makonda pia ameipongeza Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwa mapinduzi makubwa ya bandari na kuitaka kutekeleza ahadi yake ya kuhakikisha bandari hiyo inahudumia meli zenye urefu wa mita 100 kwa kukamilisha ujenzi kwa wakati.

“Tekelezeni ahadi zenu ili mkamilishe ujenzi huu mapema,” amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Salum Hamduni amesema ofisi yake itasimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ili thamani ya fedha ionekane na tija iliyokusudiwa ipatikane hasa katika kubeba ongezeko la shehena litakalotokana na SGR.

Naye Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria Bi. Rosemary Ndesamburo amesema bandari hiyo itahudumia meli 5 kwa wakati mmoja itakapokamilika, huku shirika hilo likiendelea kupanua bandari nyingine za Ziwa Victoria kama ya Bukoba.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.