Kuelekea mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, kati ya Pamba Jiji FC dhidi ya Simba SC, makocha wa timu zote mbili wamezungumza kwa tahadhari.
Kwa upande wake Kocha wa Pamba Jiji FC, Francis Baraza amesema wao kama benchi la ufundi tayari wamekamilisha maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo huku akisema Simba wana kikosi kizuri.

Naye Kocha wa Simba SC, Steve Barker Amesema kua licha ya safari kua nyingi na michezo kua karibu lakini wao tayari wamejipanga kuhakikisha wanaondoka na alama tatu katika mchezo huo kwani anafahamu ugumu na ushindani uliopo katika ligi kuu Tanzania bara.

Aida mchezaji wa Simba SC, Morice Abraham amesema kua mchezo huo utakua mgumu, kwani wazezaji wa pamba wanafahamiana vizuri hivyo hautakua mchezo rahisi kwao.
Discussion
Reader comments
0 contributions