Skip to main content

MAKAZI YA MUDA YAANDALIWA MVUA ZA EL - NINO

Mkoa wa Kagera umeweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi cha mwezi Oktoba hadiDesemba 2026, ikiwemo kuandaa maeneo ya makazi ya muda na kutenga vituo vya afya kwa ajili ya kutoa huduma za dharura.

MAKAZI YA MUDA YAANDALIWA MVUA ZA EL - NINO
Studio Narration JAMBO FM

MAKAZI YA MUDA YAANDALIWA MVUA ZA EL - NINO

0:00 --:--

Mkoa wa Kagera umeweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi cha mwezi Oktoba hadiDesemba 2026, ikiwemo kuandaa maeneo ya makazi ya muda na kutenga vituo vya afya kwa ajili ya kutoa huduma za dharura.

Mkuu wa Mkoa huo Kanali Yahaya Ramadhani Kido amesema maandalizi hayo ni sehemu ya hatua za Mkoa katika kukabiliana na maafa yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.

Amesema Kamati ya Maafa ya Mkoa imeanza kukagua maeneo hatarishi katika Wilaya ya Bukoba kwa lengo la kubaini changamoto zinazoweza kujitokeza na kuchukua hatua za kujikinga mapema.

Ukaguzi huo unalenga  maeneo yanayoweza kutumika kama makazi ya muda na vituo vya kutolea huduma za dharura yanakuwa tayari endapo kutatokea maafa.

Ameongeza kuwa  maandalizi hayo yatawezesha Mamlaka kuchukua hatua kwa wakati na kupunguza madhara kwa wananchi, ikiwemo kupoteza maisha, mali na miundombinu kutokana na mvua kubwa.

Kanali Kido amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi kuchukua tahadhari na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na viongozi na Mamlaka zinazohusika na usimamizi wa maafa.

Aidha amewataka wananchi kufuatilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini ili waweze kuchukua hatua stahiki kulingana na tahadhari zinazotolewa.

Katika hatua nyingine Kanali Kido amesisitiza umuhimu wa wanachi kutumia elimu na melekezo wanayopewa kuhusu namna ya kujikinga na athari za mvua kubwa akieleza kuwa maandalizi ya mapema ni muhimu katika kulinda maisha,mali na miundombinu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.