Skip to main content

MAKANDE, TOGWA YACHUKUA UHAI WA MTOTO 41 WAKILAZWA SINGIDA

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 15 amefariki dunia na watu wengine 41 kuugua baada ya kula makande na kunywa togwa vinavyodhaniwa kuwa na sumu katika Kijiji cha Unyambwa, Kata ya Unyambwa, Manispaa ya Singida.

MAKANDE, TOGWA YACHUKUA UHAI WA MTOTO  41 WAKILAZWA SINGIDA
Studio Narration JAMBO FM

MAKANDE, TOGWA YACHUKUA UHAI WA MTOTO 41 WAKILAZWA SINGIDA

0:00 --:--

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 15 amefariki dunia na watu wengine 41 kuugua baada ya kula makande na kunywa togwa vinavyodhaniwa kuwa na sumu katika Kijiji cha Unyambwa, Kata ya Unyambwa, Manispaa ya Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Oktoba 18, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Matride Kuyeto, amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 17, mwaka huu, majira ya saa 8:00 mchana, wakati marehemu na watu wengine 41 walipokuwa wakishiriki chakula cha makande na kinywaji cha togwa kilichoandaliwa kwa ajili ya shukrani za kazi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Oktoba 18, majira ya saa 5:00 asubuhi, marehemu pamoja na watu wengine 41 walianza kuumwa tumbo na kuishiwa nguvu. Watoto wawili kati yao walikimbizwa katika Zahanati ya Moyo wa Yesu Mangua mitogo, ambako mtoto Ridhwani Ayoub Omari, mwenye umri wa miaka 13, alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Aidha, watu wengine 40 walipelekwa Hospitali ya Manispaa ya Singida kwa ajili ya matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya uchunguzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Matride Kuyeto

Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida limetoa wito kwa wananchi wa Kijiji cha Unyambwa kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi wa chanzo cha tukio hilo ukiendelea.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.