Skip to main content

MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI ASISITIZA MALEZI KATIKA FAMILIA

Na Ibrahim Rojala, Chato - Geita.

MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI ASISITIZA MALEZI KATIKA FAMILIA

Na Ibrahim Rojala, Chato - Geita.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewataka wazazi na walezi kumuenzi mama mzazi wa Hayati Dkt. John Magufuli kwa  kuwaandaa watoto kupitia malezi bora katika kulitumikia taifa kwenye nyadhifa mbalimbali.

Balozi Dkt. Nchimbi amesema hayo leo Mei 29,2026 alipomwakilisha Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mazishi ya aliyekuwa mama mzazi wa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt.m John Magufuli, Sussana Ngolo Mussa yanayofanyika leo nyumbani kwa Marehemu wilayani Chato mkoa wa Geita.

Amesema Mama Sussana licha ya kutotokea katika familia ya wanansiasa,alitimiza wajibu wake wa malezi bora kwa familia na kuwezesha taifa kupata kiongozi mahiri na mchapakazi.

Makamu wa Rais amesema kutokana na malezi bora ya mama yake,Hayati Rais Magufuli alikuwa  na utashi wa kulea na kuandaa viongozi wengine ili waje kulitumikia taifa akitolea mfano namna Hayati Magufuli alivyomsaidia wakati alipotangaza kuachana na siasa jimbo la Njombe mjini.

Nchimbi amesema, wazazi wanao wajibu wa kulea watoto kwa kuwaandaa katika kulitumikia taifa ambapo amesema kufanya mema kwa binadamu mwenzako sio lazima yalipwe kwako.

Akitolea Mfanowa matunda yamalezi bora ya mama huyo,amesema baada ya yeye kutangaza kustaafu, Makamu Mwenyekiti wa CCM Stephen Wasira alimpigia simu akimtaka kubatilisha uamuzi wake.Baada ya Wasira Hayati Magufuli pia alimpigia simu na kumtia moyo kama mdogo wake kwa umri na baadaye kumteua kuwa Balozi nchini Brazil.

"Emmanuel mdogo wangu hivi umepata wazimu? Nani amekwambia Siasa tunastaafu? Wewe unakuwa mpinzani wa demokrasia, unapogombea ukashinda unashukuru na ukishindwa unashukuru na uchaguzi ujao unarudia tena, sasa mambo gani unaanzisha?"

Ameongeza kwamba Baada ya simu ya Wasira,aliyefuata kumpigia simu alikuwa Hayati Dk Magufuli aliyemtaka kuachana na uamuzi wa kuachana na siasa kwakuwa umri wake ulikuwa bado mdogo.

"Mtani hivi niliyoyasikia ni kweli au wanasema uongo? Unapumzika siasa? Nikamwambia ni kweli,akasema (Magufuli) katika umri huo mimi sijapumzika na nimekuzidi miaka kumi"

Balozi Dkt. Nchimbi amesema hayati Magufuli alimwambia akishinda urais angempatia nafasi ya ubunge kati ya nafasi 10 alizonazo kikatiba za uteuzi wa wabunge hatahivyo hakuwa tayari.Ameongeza kuwa baada ya uchaguzi mkuu kupita,alikaa mwaka mzima nje ya siasa hali iliyomfanya kumpigia tena simu akitaka kufahamu ikiwa amebadili uamuzi wa kupumzika.

"Hayo mapumziko hayajaisha mtani?Nikamwambia hapana,nimeamua kupumzika siasa," alisema.

Baada ya kauli hiyo,Hayati Magufuli alimteua Balozi Dk Nchimbi kuwa Balozi nchini Brazil, nafasi ambayo amesema azingeweza kupinga uteuzi wa Rais.

Pia Balozi Dk Nchimbi amesema Hayati Magufuli hakupenda kukomaa na jambo fulani kama wengi wanavyodhani,badala yake alipenda mabishano yenye hoja ambapo Makamu wa Rais alipenda kubishana naye hata walipokuwa wakikaa pamoja bungeni kwa miaka mitatu.

Aidha Balozi Dk Nchimbi amesema Hayati Magufuli amegusia ujumbe aliotumiwa na kiongozi huyo wa kumtia moyo baada ya kuteuliwa nafasi ya ubalozi.

"Mungu atakusaidia,siwezi kukutupa mdogowangu nilikwisha ahidi kwamba Mimi ni pamoja na wewe,haijalishi yaliyopita yamepita,wewe bado ni kijana siwezi kuharibu future yako,natambua kazi nzuri ulizofanya kwa nchi hii,kutofautiana mawazo na kubishana bishana sio uadui,salam kwa familia" Ulisema ujumbe huo aliotumiwa Dk Nchimbi na hayati Magufuli.

Naye Askofu wa jimbo katoliki la Bunda Simon Masondole akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya baraza la Maaskofu katoliki,TEC ametoa wito kwa jamii kumuenzi Mama Sussana kupitia malezi bora na kuendelea kuliweka taifa katika umoja.

Akitoa salam za shukrani kwa niaba ya familia,Simon Michael ameishukuru Serikali ya awamu ya sita,madaktari na wahudumu wa afya pamoja na wananchi kwa kuwa na familia kwa nyakati zote za kumuuguza Marehemu.

Marehemu Sussana Ngolo Mussa ambaye ni mama mzazi wa Rais wa awamu ya tano Hayati Dk John Magufuli,alifariki jioni ya Mei 25,2026 baada ya kusumbuliwa na tatizo la moyo,kisukari na shinikizo la damu kwa muda mrefu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.