Makampuni yanayonunua Tumbaku na taasisi za kibenki zinazowakopesha wakulima katika mkoa wa kitumbaku Kahama wameungana na Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) kuwahamasisha wakulima wa zao hilo kurudi Shambani na kuendelea na kilimo.
Wakiwa katika Kata za Ulowa,Ubagwe na Bulungwa kampuni hizo zimetumia mikutano hiyo ya semina kuwasihi wakulima kutokata tamaa kulima zao la tumbaku kutokana na hali ya soko lilivyokuwa msimu uliopita.
Akizungumza kwa niaba ya makampuni mengine ya Ununuzi meneja wa kampuni ya Global Leaf Jofrey Biya amewataka wakulima kuongeza nguvu katika kilimo cha zao hilo kwakuwa kampuni nyingi zinahitaji Tumbaku na wameongeza wastani wa mahitaji ya zao hilo katika kampuni zao.
"Msimu 2026/2027 ndugu zangu una neema kubwa,mahitaji ya Tumbaku yameongezeka sana kwa makampuni lakini pia kuna ongezeko la makampuni mengine mapya ambayo yanahitaji Tumbaku,hivyo twendeni turudi shambani kwa nguvu zote neema ipo"Amesema Biya.
Katika hatua nyingine Biya ameongeza kwa kuwataka wakulima kwenda kuzingatia maagizo ya wataalamu ili kuhakikisha wanazalisha tumbaku zenye ubora.
"Niwaombe sana ndugu zangu wakulima nendeni mkazingatie maagizo yote mnayopewa na wataalamu hususan suala la mvua za El-nino mkazingatia yote mliyoelekezwa na wataalam" Amesisitiza Biya.

Naye Afisa mahusiano wa kampuni ya Jespani Charles Gasper amesema kuwa katika msimu huu 2026/2027 wana uhitaji mkubwa wa tumbaku hivyo ni jukumu la wakulima kurudi shambani na kuzalisha tumbaku nyingi na yenye ubora.
"Tuwahakikishie wakuli Sisi Jespan na makampuni mengine ya ununuzi tuna uhitaji mkubwa sana wa Tumbaku,hivyo wakulima niwaombe sana rudini shambani mkazalishe Tumbaku bora bila kukata tamaa" Amesema Gasper
Kwa mujibu wa Bodo ya Tumbaku Tanzania (TTB) mkoa wa kitumbaku Kahama unatarajia kukusanya kilo milioni 27 kwa msimu wa 2026/2027.
Discussion
Reader comments
0 contributions