Skip to main content

MAGEUZI YA KIUCHUMI YAAKISI MAISHA YA WANANCHI - DKT. SAMIA

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema mageuzi yanayofanyika kwenye sekta ya fedha yanapaswa kuakisi maisha halisi ya wananchi, si kubaki katika takwimu.

MAGEUZI YA KIUCHUMI YAAKISI MAISHA YA WANANCHI - DKT. SAMIA

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema mageuzi yanayofanyika kwenye sekta ya fedha yanapaswa kuakisi maisha halisi ya wananchi, si kubaki katika takwimu.

Dkt Samia ameeleza hayo leo Juni 12, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Ameeleza kuwa mageuzi yanayoyazungumza ni muhimu lakini kama hayatabadili maisha ya wananchi yatasalia kuwa takwimu katika ripoti.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Takwimu zitasema kama tunvyoona upande kwingine, uchumi unapanda, GDP ni kubwa, uchumi wa nchi ni mkubwa lakini ukifika kwa watu hali za watu siyo nzuri,” ameeleza Dkt Samia na kuongeza kuwa;

“Msiposimamia vema, mabadiliko hayo yatabaki kuwa takwimu na ni vema kutafsiri ukuaji wa uchumi ili uende ukakue mpaka kwa mtu wa kawaida kule chini,” amesema.

Amefafanua kuwa mafanikio katika mifumo wa fedha hayana budi kwenda na mafanikio ya mwananchi mmoja.

Dkt Samia kipimo kisibaki kuwa ni wananchi wangapi wamefikiwa na huduma ya fedha, bali kiwe ni kwa kiasi gani huduma za fedha zinakuza mitaji na biashara ndogondogo na kuweza kuchangia kuwafanya wale wa biashara ndogondogo kuchangia katika uchumi wa nchi.

Katika hatua nyingine, Dkt Samia amezitaka taasisi za fedha nchini kuwa wabunifu katika kutafuta njia zitakazowawezesha kutoa mikopo kwa wananchi bila kuhitaji dhamana zilizozoeleka kama nyumba, gari au kiwanja, bali watumie uaminifu wao katika bishara wanazozifanya.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.