Skip to main content

MAGANYA ATAKA VIKUNDI VITENGENEZEWE KATIBA, OFISI YA MKURUGENZI

Na Afarah Suleiman, Hanang' - Manyara.

MAGANYA ATAKA VIKUNDI VITENGENEZEWE KATIBA, OFISI YA MKURUGENZI
Studio Narration JAMBO FM

MAGANYA ATAKA VIKUNDI VITENGENEZEWE KATIBA, OFISI YA MKURUGE...

0:00 --:--

Na Afarah Suleiman, Hanang' - Manyara.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhili Maganya ameagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, kuhakikisha wanawatengenezea katiba vikundi vya wananchi vinavyojitokeza kuomba mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri bure badala ya kuwakosesha fursa ya mikopo hiyo kwa kigezo cha kikundi kukosa katiba.

Maganya ametoa agizo hilo, kwa halmashauri hiyo na nyingine nchini wakati akizungumza na wananchi na Wana CCM Wilayani Hanang katika ziara yake ya kikazi ambayo anaianza ndani ya mkoa wa Manyara na kuitaka CCM na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Hanang, kufuatilia kwa karibu michakato ya utoaji wa mikopo hiyo

Aidha, Mwenyekiti huyo ametoa pia wito wa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya mvua zinazotarajiwa kunyesha nchini licha ya mamlaka ya hali ya hewa kuonyesha mvua hizo zitanyesha kwa siku kumi kwa baadhi ya maeneo.

Ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Maganya Mkoani hapa ni ya kikazi ambapo pia ametembelea miradi na kufanya vikao vya uimarishaji wa Chama cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi wa ndani ya Chama hicho mwaka ujao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.