Na Afarah suleiman, Mererani - Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Fakii Lulandala ameipongeza kampuni ya Permanent Mineral Limited kwa kuwagusa wananchi zaidi ya 1000 wa mji mdogo wa mererani walio kumbwa na mafuriko kwa kuwapatia misaada mbalimbali ya kibinadamu.
Ameyasema hayo baada ya kupokea msaada huo kwa niaba ya Wananchi wa mji mdogo wa Mererani, waliokumbwa na mafuriko, ikiwemo chakula, sabuni, mafuta pamoja na vifaa mbalimbali vya shule vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milion 22.

Kwa upande wake Msimamizi wa Kampuni ya Permanent Mineral Llimited na Mwenyekiti wa Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara, Elisha Mnyawi baada ya kukabidhi msaada huo , wametoa wito kwa Wachimbaji na Taasisi nyingine zikiwemo za dini kujitokeza katika kuwasaidia wahanga wa mafuriko hayo.


Baadhi ya wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo, wameiomba serikali kuongeza mitaro midogo kwenye makazi yao, ili kuondokana na hadha hiyo ya mara kwa mara.



Discussion
Reader comments
0 contributions